
Bwana Khashoggi, mkosoaji maarufu wa Saudi arabia, aliuawa katika ubalozi mdogo wa Saudia mjini Istanbul oktoba 2018.
Idara ya ujasusi ya Marekani imesema inaamini mwanamfalme Mohammed aliamuru mauaji hayo.
Lakini katika kesi iliyowasilishwa mahakamani, wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema ana kinga kutokana na jukumu lake jipya kama waziri mkuu wa Saudi arabia.
Mchumba wa zamani wa Bw Khashoggi, Hatice Cengiz, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba "Jamal amefariki tena leo" kutokana na uamuzi huo.
Yeye pamoja na shirika la kutetea haki za binadamu la Democracy for the Arab World Now (Dawn), lililoanzishwa na Bw Khashoggi walikuwa wakitafuta uharibifu usiojulikana nchini Marekani kutoka kwa mwanamfalme huyo kwa mauaji ya mchumba wake.