
kipimo cha UKIMWI
Wakizungumza wakati wa kutoa taarifa kwa umma kuhusu maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani ambapo kitaifa yatafanyika Mkoani Lindi, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS anasema, jumla ya watu milioni 1 na laki 7 ni waathirika wa VVU nchini, huku maambukizi mapya yakipungua kwa asilimia 50 kutoka watu laki 1 na 10 mwaka 2010, hadi watu elfu 54 kwa mwaka 2021 lakini, idadi ya maambukizi mapya inaonekana zaidi kwa vijana hasa wanawake.
Takwimu ya mwaka 2017 ya ugonjwa wa UKIMWI inaonyesha mkoa wa Lindi ndio mkoa wenye idadi ndogo ya maambukizi ikiwa na asilimia 0.3, kwasababu ya kuwepo miradi mikubwa kama wa kuchakata gesi asilia na mingine Mingi, wananchi wanaaswa kuchukua tahadhari kubwa kwani ugonjwa huo hushamiri zaidi maeneo yenye muingiliano wa watu wengi.
Disemba mosi maadhimisho ya siku hii kubwa yatafanyika mkoani Lindi ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.