
Mmoja wa wananchi waliopatiwa huduma
Wakizungumza baada ya kupatiwa matibabu baadhi ya wagonjwa wakiwemo wale waliofanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho wamepongeza kazi kubwa inayofanywa na madaktari hao kutokana na afya zao kuanza kuimarika.
Mratibu wa zoezi hilo Ragib Hasanal pamoja na Mganga Mkuu wa hospitali ya Msoga Dkt. Allen Mlekwa, akielezea ujio wa madaktari hao utakavyosaidia kupunguza adha ya wagonjwa waliokua wakihitaji matibabu ya kibingwa.