Wednesday , 14th Dec , 2022

Shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR kwa kushirikiana na Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma imezindua mpango wa pamoja wa kuhakikisha vifaa vya TEHAMA vinapatikana kwa mahakama zote za wilaya kwa lengo la kuwezesha utatuzi wa kesi mbalimbali kwa njia ya mtandao

Akizunguza katika hafra ya makabidhaino ya vifaa vya tehama Jaji mfawidhi mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma  Lameck Mlacha amesema upatikanaji wa vifaa hivyo ni hatua muhimu katika kuhalakisha kumaliza mashauri mbalimbali ya jinai

Kwa upande wake afisa hifadhi mwandamizi shirika la kimataifa la kuhudumia wakimbizi mkoa wa Kigoma Peter Muriuki amesema vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni baada ya mahakama kuhitaji vifaa hivyo, huku baadhi ya wadau wa sheria wakieleza tija zaidi kutokana na upatikanaji wa vifaa vya tehama katika maeneo ya kazi