
Taarifa ya kitengo cha mawasiliano ya serikali imeeleza kuwa mwili wa balozi huyo utasafirishwa kesho Jumamosi Disemba 17/2022 kutoka hospitali ya wilaya ya Handeni kwenda Moshi kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika Jumanne katika kijiji cha Sambarai kata ya Kindi, tarafa ya Kibosho, Moshi vijijini
Balozi Mushy alifariki dunia Disemba 12/2022 katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Mkata wilayani Handeni baada ya gari alilokuwa anaendesha kugongana na lori na kuungua moto
Balozi Mushy aliteuliwa na Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa balozi wa Tanzania nchini Austria na mwakilishi wa kudumu katika Ofisi ya umoja wa Mataifa Vienna mwezi Januari mwaka 2022