Wednesday , 21st Dec , 2022

Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), imetangaza rasmi kuanza kwa usajili wa vitambulisho vya Taifa kwa njia ya mtandao, ili kupunguza msongamano wa watu katika ofisi za usajili ngazi ya wilaya.

Vitambulisho vya NIDA

Akizungumza leo, Msemaji wa NIDA Geofrey Tengeneza amebainisha kuwa watu wengine wamekuwa wakipoteza muda mwingi kujisajili hali inayopunguza mwamko wa watu kujisajili.

Aidha Tengeneza amebainisha kuwa mfumo huu wa njia ya mtandao, hautawahusu waliopoteza vitambulisho vyao au ambao vitambulisho vyao vinaisha muda wake.

NIDA wameeleza kuwa wamekuwa wakitumia gharama kubwa kwenye uzalishaji wa fomu na kusimamia zoezi la usajili kwa njia kawaida, hivyo kwakutumia mtandao, itasaidia kupunguza kero kwa watu hasa kipindi hiki ambacho kitambulisho hicho kimekuwa na uhitaji mkubwa.