
Mlinda Mlango Andre Onana
Onana alikua golikipa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Cameroon katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2022 nchini Qatar, na alicheza mchezo dhidi ya Uswizi waliopoteza kwa goli 1-0.
Alikosana na Kocha Mkuu wa kikosi hicho Rigobert Song wakati huo wa michauno ya Kombe la Dunia nchini Qatar na kuondolewa katika kikosi hicho kisha alirejeshwa nyumbani na Song akisema alifikia maamuzi hayo kutokana kukiuka maelekezo na utovu wa nidhamu kwa mlinda mlano huyo wa klabu ya Inter Milan.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 26 alianza soka lake katika akademi ya Samuel Etoo na kucheza mechezo wake wa kwanza wa kimataifa wa kirafiki walioshinda mabao 2-1 dhidi ya Gabon.
Kwenye taarifa yake Onana alisema kila hadithi hata iwe nzuri kiasi gani huwa ina mwisho wake. Na hadithi yake na timu ya taifa ya Cameroon ndio imefikia hatua hii.Wachezaji huja na kuondoka, lakini maslahi ya Cameroon mara zote ndio muhimu kuliko mchezaji yoyote, hivyo atabaki kuwa shabiki na kupeperusha bendera ya nchi hiyo popote aendapo.