Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Madereva 17 wa magari ya IT wakamatwa

Thursday , 29th Dec , 2022

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawashikilia madereva 17 wa magari yanayosafirishwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda nje ya nchi (IT) kwa kosa la kusafirisha abiria kinyume cha sheria ya usalama barabarani sura ya 168 inayokataza magari hayo kusafirisha abiria

Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Pius Lutumo pamoja na mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Edson Mwakihaba wamesema Magari hayo ya IT yanayoanzia safari  zao Bandari ya Dar es salaam kwenda nchi za Zambia, Rwanda, Burundi na Congo kupita mikoa ya Pwani, Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, Geita na Kagera yamekuwa yakisababisha ajali na kuleta madhara makubwa kwa abiria, hivyo hii ni operesheni endelevu ili kuzuia biashara hiyo hatarishi.

Wito wa Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani ni kuwataka abiria kutumia usafiri rasmi wa umma ili kuepusha usumbufu wanaoweza kuupata safarini kwa kukosa haki zao za msingi inapotokea ajali watumiapo magari ya IT. 

Aidha amewataka madereva wanaoendelea kukaidi na kuvunja sheria ya usalama barabarani kwa makusudi kuacha mara moja kwani jeshi la polis litaendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwemo kukamatwa na kufikishwa mahakamani  

HABARI ZAIDI

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini

Rose Senyagwa, Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka TMA

Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari