Saturday , 14th Jan , 2023

Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi CCM imemteua Sophia Mjema kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho akichukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka

Aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM Shaka Hamdu Shaka amewashukuru wanahabari kwa ushirikiano wao ndani ya chama hicho hususani wakati wa uchaguzi

Shaka ametoa kauli hiyo wakati akikamilisha kutangaza safu mpya ya uongozi wa Chama hicho iliyochaguliwa leo na Halmashauri kuu ya taifa 

"Niwashukuru wanahabari wote kwa mchango wenu ambao mmeutoa kwa chama kwa kipindi chote hasa kipindi cha uchaguzi mmekuwa na sisi karibu mno mpaka leo tunakamilisha safu hii mmefanya kazi nzuri sana, tunasema kazi inaendelea kwa speed na viwango" 

Katika safu hiyo mpya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imemteua Sophia Mjema kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi akichukua nafasi ya Shaka Hamdu Shaka

Shaka ametangaza majina ya kukamilisha safu ya uongozi wa chama hicho ambapo kwa upende wa Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa

Daniel Chongolo  ameendelea kuwa Katibu Mkuu huku Anamringi Macha  akichaguliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara

Kwa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Chama kimemteua Said Mohamed Dimwa huku Dkt. Frank Haule akichaguliwa kuwa Katibu wa Uchumi na Fedha

Mbarouk Nassor Mbarouk amechaguliwa kuwa Mkuu wa Idara ya Kimataifa huku Issa Haji Gavu akichaguliwa kuwa Idara ya Organaizeisheni ya Chama hicho