Saturday , 4th Feb , 2023

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye ni mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku, maarufu kwa jina la Msukuma, amewataka Wakuu wa wilaya kurekebisha bei za vyakula ili zipungue na kuwawezeaha wananchi kununua vyakula kwa bei nzuri.

Mbunge wa jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku

Msukuma ametoa kauli hiyo jijini Mwanza kwenye maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi na kuwataka Wakuu hao wa wilaya wadhibiti wakulima na wale wanaoleta mazao kuuzwa sokoni wasipandishe bei.

"Mfumuko wa bei unaitesa Tanzania, tunanunua mchele 3500 ukiwauliza watu wanakuambia Covid mara Ukraine, wakuu wa wilaya mpo rekebisheni hizi bei," amesema Msukuma