Sunday , 5th Feb , 2023

Wazazi wa watoto waliokuwa wanasoma katika shule ya sekondari Thaquafa iliyopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza wameandamana kudai matokeo ya watoto wao waliomaliza kidato cha nne mwaka jana kufuatia kuwepo kwa sintofahamu

Wazazi hao wamesema wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana katika shule hiyo walikuwa 164 matokeo ya mtihani yametoka ya wanafunzi 22 pekee wengine matokeo yao hayajulikani yalipo 

‘Hatujui Watoto wetu tunawapeleka wapi tunamlilia Rais wetu Samia Suluhu huko aliko atuangalie kwa hii shule ya Thaqafa sisi wengine ni wajane tunahangaika na Watoto wetu wa kike tunawapeleka wapi sisi Watoto hawa" 

Afisa Elimu sekondari wa halmashauri ya jiji la Mwanza Allan Said amefika katika shuel hiyo na kuzungumza na wazazi wa wanafunzi hao na kuwataka kufuata taratibu zote za madai yao

"Serikali inafanya kazi kwa kutumia makaratasi wewe ukisema mimi mtoto wangu amefutiwa utalizwa Ushahidi uko wapi nyie chukueni barua muende nazo mkaulize vizuri kuhusu hayo matokeo ya Watoto wenu"