Wednesday , 8th Feb , 2023

Zaidi ya hekari 72 za mahindi, 30 za parachichi na nyumba 15 za wananchi wa Kijiji cha Image, Kata ya Kidegembye zimeharibiwa vibaya na mvua iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali na mawe huku ikiacha vilio kwa baadhi ya wananchi hao kubaki bila chakula na makazi.

Mmoja wa wananchi walioathiriwa na mvua

Wananchi wa Kijiji hicho wanasema wanashangaa mvua hiyo kunyesha kwani haijawahi kutokea katika maisha yao huku, Mbunge wa jimbo la Lupembe Edwin Swale akilazimika kutoa msaada wa mabati 100 ili kuwanusuru wananchi waliokosa makazi.

Mazao yaliyoharibiwa

Aidha wananchi hao wameiomba serikali kuwasaidia msaada wa chakula na makazi ambapo Katibu Tawala wilaya ya Njombe amefika kijijini hapo na kujionea hali halisi ilivyo huku akiwaahidi wananchi hao kusaidiwa haraka iwezekanavyo.