Wednesday , 15th Feb , 2023

Serikali ya Tanzania kupitia wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuingia makubaliano na India kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha masuala ya tehema ili kuongeza tija katika sekta hiyo ikiwa ni matokeo ya ziara kadhaa zilizofanywa nchini India.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda

Mapema hii leo (February 15,2023) waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia prof Adolf Mkenda Amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya watalaam kutoka India wakiongozwa na balozi wa India nchini Tanzania Bihaya pradhan ambao wamelenga kutembelea vyuo kadhaa hapa nchini kwa ajili ya kuona maeneo ambayo wao wanaweza kuwekeza.

“Tayari serikali ya Zanzibar imekwisha andaa eneo kwa ajili ya uwekezaji huo ikilinganishwa kuwa masuala ya elimu ni masuala ya muungano hivyo chuo hicho kujengwa popote ni sawa kwa mujibu wa sheria na tataratibu”.amesema Prof Mkenda.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji ama kuwa na mmifumo ya kuwaandaa watalaam kuweza kustahilimi soko la ajira katka dunia ya Tehama kwenye sekta ya uwekezaji