Monday , 27th Feb , 2023

Muuzaji mkubwa wa dawa za kulevya nchini Thailand alifanyiwa upasuaji wa plastiki usoni  mara kadhaa  ili kuonekana kama  mtu muungwana tena mwenye uraia wa  Kikorea ili na kukwepa sheria, mamlaka za eneo hilo zimesema.

Saharat Sawangjaeng,   alikamatwa wiki iliyopita  huko Bangkok.  Polisi, ambao walikuwa wakimsaka kijana huyo mwenye umri wa miaka 25 kwa miezi mitatu, walisema  hana sura yake ya awali . Walimfuatilia kwa kufuatilia usambazaji wa dawa hizo kwa wauzaji wengine na wanunuzi huko Bangkok.

Walioshuhudia walimtaja kama mtu mwenye muonekano mzuri wa Kikorea . Pia alikuwa amebadilisha jina lake kuwa la Kikorea. Katika video ya kukamatwa kwake iliyotolewa na polisi, Bw Saharat alisema anataka kuhamia Korea Kusini na kwamba amechoka kuishi  Thailand.

Bw Saharat ameshtakiwa kwa kuingiza dawa za kulevya kinyume cha sheria. Alikiri kuagiza MDMA - ambayo pia inajulikana kama ecstasy