Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Tanzania mwenyeji mkutano wa masuala ya chakula

Thursday , 16th Mar , 2023

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano mkubwa wa Afrika wa masuala ya chakula na kilimo utakaofanyika Septemba 5 mpaka 8 mwaka huu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan

Kesho Machi 17, 2023 Rais Samia Suluhu Hassan, atazindua maandalizi ya mkutano huo Ikulu, Dar es Salaam, hii ni kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Zuhura Yunus.

Mkutano wa Afrika wa chakula wa Septemba unatarajiwa kuhudhuriwa na watu takribani 3,000 kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika na duniani, ikiwemo Marais, Mawaziri na wakuu wa taasisi za kimataifa.

Mkutano huo utaweka msisitizo kwenye vijana na wanawake kama msingi wa mfumo endelevu wa chakula.

Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na hatua kubwa za kimageuzi ambazo serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imezichukua tangu alipoingia madarakani miaka miwili iliyopita.

Hatua hizo ni pamoja na kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa mara nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu Uhuru upatikane.

Serikali ya Rais Samia pia imetambuliwa kwa mradi wake wa ubunifu wa Jenga Kesho Iliyo Bora (BBT), ambao unalenga kuwawezesha vijana, ambao ndiyo nguvu kazi kubwa nchini, kuingia katika kilimo.

Serikali yake pia imewekeza kwenye miundombinu ya umwagiliaji, huduma za ugani, pembejeo na ruzuku ya mbolea na mbegu kwa viwango ambavyo havijawahi kufanyika miaka ya nyuma.

Serikali pia imekuwa ikitekeleza mpango wa kilimo unaojulikana kama Ajenda 10/30 yenye lengo la kufanya kilimo kiwe cha biashara na kikue kwa wastani wa asilimia 10 kwa mwaka ifikapo 2030.

 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo

Wanafunzi 194 washika mimba ndani ya mwezi mmoja

Mabaki ya gari aina ya Noah iliyopata ajali Morogoro

Ajali yachukua uhai wa watu saba Morogoro

Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Wawekezaji wawekeze sekta za uzalishaji - Nchemba

Muonekano wa Kiburugwa ambako Nyumba zaidi ya Tisa Zimebomolewa na Maporomoko ya Tope

Maporomoko ya udongo yasomba nyumba 9 Mbagala

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko

Serikali yaipongeza Red Cross

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa