Thursday , 30th Mar , 2023

Watu wawili wamenusurika kifo baada ya gari aina ya lori la Kampuni ya Pepsi walilokuwa wamepanda kuanguka likiwa na soda Kiteto mkoani Manyara leo Machi 30.2023 

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara George Katabazi amesema ajali hiyo imesababishwa na kufeli breki

Amesema gari hilo lilikuwa linatoka Mjini Kibaya kuelekea barabara ya Dodoma nusu km na kuanguka eneo la darajani

Manusura wa tukio hilo ambao majina yao hayajafahamika mapema walitoweka baada ya ajali na Jeshi la Polisi linaendelea na taratibu za upelelezi.