Wednesday , 12th Apr , 2023

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imesema katika kipindi cha mwezi julai mpaka desemba 2022 iliweza kukamata bidhaa zilizoingia nchini kwa njia ya Magendo zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni ni 11 kabla ya kodi ikilinganishwa bidhaa za magendo zilizokamatwa nchi nzima Mwaka 2021.

Yamesemwa hayo na Kamishna Mkuu wa TRA Alphayo kidata wakati akipokea boti mbili za kisasa za doria kwa ajili ya kuimarisha udhibiti wa uingizwaji wa bidhaa za magendo nchini katika ukanda wa pwani na kigoma

Akizungumza, Kamishna mkuu huyo amesema bidhaa za magendo zimekuwa zikififiza uchumi wa nchi , kuhatarisha Afya za walaji na hata kurudisha nyuma maendeleo ya viwanda

'Leo tumepokea boti mbili yakiwa ni matokeo mazuri Takribani shilingi bilioni 2.5 zili idhinishwa kwenye bajeti ya mwaka 2021/2022 kwa ya manunuzi ya boti tatu ambapo boti mbili zimekabidhiwa huku moja ikipata hitilafu wakati wa kuishusha lakini itakuwa sawa'ameongeza Kidata.