
Wakizungumza na #EATV wakazi hao ambao wengine maji yameingia mpaka ndani ya nyumba hizo wamesema chanzo ni kuwepo kwa mto mdogo kwenye makazi yao ambapo mvua inaponyesha maji yamekuwa yakitirika katika mto huo badala ya kwenda moja kwa moja mto Ng"ombe
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Magomeni Makanya Chano Chano amesema wananchi hao wamekuwa wakiishi kwa hofu na wasiwasi mkubwa kila mara mvua inaponyesha
Naye diwani wa kata ya Ndugumbi ambaye ndie anayesimamia eneo hilo Thadei Masawe ameeleza mpango wa halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni uliopo kwa sasa katika kuliendeleza eneo hilo Ili lisiendelee kuathiri makazi ya watu kwa maji kuingia kwenye nyumba zao