Sunday , 7th May , 2023

Watu 182 wameripotiwa kufa kutokana na mafuriko na maporomoko makubwa ya ardhi katika eneo la mashariki ya Kongo. Mamlaka mashariki mwa DRC zinasema kuwa idadi hiyo inazidi kuongezeka.

Theo Ngwabidje, Gavana katika eneo hilo amethibitisha vifo vya watu hao kwa shirika la Habari la Ujerumani (dpa ) na kusema kuwa huenda vifo zaidi vikaripotiwa, huku wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu nchini DRC, wamepata miili hiyo wengi wakiwa wanawake na watoto katika kijiji cha Bushushu, mashariki mwa nchi hiyo.

Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi, ametangaza rasmi kuwa siku ya jumatatu itakua siku maalum ili kuomboleza kama taifa .

Maombolezo haya yanafanyika wakati huu Serikali ikiendelea kukadiria hasara iliyotokana na mafuriko hayo, huku shughuli za mazishi pia zikiendelea katika moja ya majanga mabaya zaidi kuwahi kuikumba nchi hiyo.

Aidha wengine mbali na kupoteza ndugu zao, wamesema shughuli za maisha ya kawaida zimekoma rasmi baada ya kupoteza mali nyingi ambazo walikuwa wakizitegemea kukimu familia zao.