Monday , 15th May , 2023

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajia kukutana na kamati ya wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo, Mawaziri wa sekta husika na Mamlaka ya Mapato Tanzania ( TRA).

Hatua hiyo inakuja baada ya wafanyabiashara hao kutangaza kuanza mgomo katika soko hilo wakidai kuwa wana malalamiko yao dhidi ya mamlaka jambo ambalo limeleta usumbufu mkubwa sokoni hapo

Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Saa 8 Mchana kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu MAGOGONI- ikulu
Jumatano tarehe 17 Mei 2023 kwa unaratibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala.

Taarifa yaWaziri Mkuu imeelekeza kuwa kwa sasa wafanyabiashara wa soko hilo waendelea na shughuli zao za biashara wakati Serikali inajiandaa kukutana nao kwa lengo la kuwasikiliza na kushughulikia kero zinazowakabili.