Wednesday , 2nd Aug , 2023

EWURA imesema kwamba kupanda kwa bei ya mafuta mwezi Agosti yanatokana na changamoto za upatikanaji wa dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya shilingi dhidi ya dola, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.

Dola ya Marekani

Hivyo bei ya petroli kwa mkoa wa Dar es Salaam itauzwa kwa shilingi 3,199, Dizeli itauzwa kwa shilingi 2,935 na Tanga petroli itauzwa kwa tsh 3,245 dizeli 2,981 na mkoani Mtwara petroli itauzwa kwa shilingi 3,271 na dizeli shilingi 3,008.

Bei hiyo mpya itaanza kutumika kesho Agosti 2, 2023.