Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Bei ya mafuta mwezi Machi yapaa

Wednesday , 6th Mar , 2024

Bei ya mafuta kwa mwezi Machi imepanda ambapo kwa  mkoa wa Dar es Salaam petroli itauzwa kwa shilingi 3,163 kutoka 3,051 mwezi Februari, dizeli 3,126 kutoka 3,029 na mafuta ya taa yatauzwa shilingi 2,840 kwa lita kuanzia leo Machi 6, 2024.

Pampu

Mkoani Tanga petroli itauzwa shilingi 3209, dizeli 3173 na mafuta ya taa yatauzwa kwa shilingi 2886 na mkoani Mtwara petroli itauzwa shilingi 3155, dizeli 3070 na mafuta ya taa yatauzwa shilingi 2913 kwa lita

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi huu yamechangiwa na ongezeko la bei za mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia (FOB) kwa wastani wa asilimia 4.5 kwa mafuta ya petroli na asilimia 1.99 kwa mafuta ya dizeli na kupanda kwa gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) kwa Bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa 15.38 kwa petroli na asilimia 40.41 kwa dizeli na kwa Bandari ya Mtwara kwa wastani wa asilimia 7.61 kwa petroli na dizeli.

EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta yamechangiwa pia na ongezeko la matumizi ya EURO katika kulipia mafuta yaliyoagizwa.

HABARI ZAIDI

Bw. Nazar Nicholas (katikati) akikabiziwa tuzo ya WSIS 2024

Tanzania yashinda Tuzo WSIS 2024, nchini Uswisi

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Anton Sabasaba Akizungumza wakati alipohudhuria kikao cha wazazi katika Shule ya Msingi Elisabane Mei 24, 2024

Wototo wafuatiliwe na kulindwa kama mboni - Anton