Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wanafunzi 80,000 wakosa masomo kisa mafuriko

Tuesday , 23rd Apr , 2024

Zaidi ya wanafunzi 80,000 wa shule za msingi katika wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani wamekosa masomo kufuatia mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Ofisa Elimu mkoa wa Pwani, Sara Mlaki, ameyasema hayo kwenye ziara ya kujionea athari za mvua hizo katika shule na makazi katika wilaya za Rufiji na Kibiti ikiwamo kuharibu  miuondombinu ya elimu.

Amesema shule 11  za msingi zenye wanafunzi 7,264 wakiwemo wasichana 3,657 na wavulana 3607 wameathirika na mafuriko wilayani Rufiji.

Aidha nyumba 58 za walimu pia zimeathiriwa na kupoteza samani na mali zilizokuwemo ndani ya nyumba hizo.

Amesema katika  wilaya ya Kibiti wanafunzi 824 katika shule 7 za msingi zimeathirika huku 3 zikifungwa kutokana na adha hiyo huku sekondari ya Mtanga Delta  ikiathirika pia.
Akizungumzia maafa hayo, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolph Mkenda, alisema tayari serikali imeweka utaratibu kwa wanafunzi wote waliokumbwa na mafuriko hayo kusoma kwenye shule maalum ambazo zimetengwa.
 
HABARI ZAIDI

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini

Rose Senyagwa, Mchambuzi wa Masuala ya Hali ya Hewa kutoka TMA

Kimbunga "IALY" kinazidi kusogea Pwani ya bahari