Friday , 6th Sep , 2024

Wenye nyumba wamekuwa changamoto na sababu ya wananchi wanao panga kutokuwa na makazi ya muda mrefu kwa kupandisha kodi.

Nyumba

Kwa upande wake mmoja wa mwananchi wa mtaa wa Biafra amesema kuwa sababu inayowafanya kuwa wanahamahama ni kukuta mazingira mabovu na nyumba kuwa mbovu hasa kipindi cha mvua na kusababisha wao kuhama.

"Kama huku sasa hivi mvua zimenyesha maji yanaingia ndani, mapaa yanafumuka, maji machafu yanaachiwa barabarani kwahiyo inakuwa kero kwa watu ndomana inakuta watu wanahama," Gilbert Jackson, Mkazi wa Mtaa wa Biafra

Zaidi wananchi wa mtaa huo wamesema kuwa changamoto inayosababisha kutotulia katika nyumba moja ni kipato kuwa chini huku Kodi za nyumba kuwa kubwa na kubadili mikataba kwa kuongeza kodi pale wanapohamia.

"Wananchi wanahama mara kwa mara, wenyenyumba utakuta labda mwezi huu unaambiwa labda utoe shilingi elfu hamsini halafu mwezi ujao anamwambia labda elfu sabini unakuta kifedha kwa muda ule hana maisha ni magumu kwaiyo unakuta mtu anahama labda mtaa wa sekenke kwenda mtaa wa Wibu” amesema Mwanahamisi Habii Musa, Mkazi wa Mtaa wa Kinondoni Mjini.