Thursday , 15th May , 2025

Baada ya tetesi kusambaa kuhusu mchezo wa mkondo wa pili Kombe la shirikisho barani Afrika kupigwa Uwanja wa Amaan Zanzibar, Klabu ya RS Berkane imethibitisha kupitia mtandao wao wa kijamii wa Instagram kuwa mchezo huo utapigwa New Amaan Zanzibar Mei 25/2025 badala ya Uwanja wa Mkapa.

Uwanja wa Amaan Zanzibar

Taarifa za mapema hii leo zilieleza kuwa  Shirikisho la soka barani Afrika ( CAF) limeliagiza shirikisho la soka nchini Tanzania ( TFF) kuhamishia maandalizi ya mchezo wa fainali ya kombe la shirikisho mnamo 25/5/2025 baina ya Simba dhidi ya Berkane kupigwa kwenye dimba la Amaan visiwani Zanzibar.

Berkane wameeleza kuwa "Uwanja wa Amaan Zanzibar utapigwa mchezo wa marudiano Kombe la shirikisho la Afrika "

Wakati huo huo Simba kupitia mitandao ya kijamii wamesema kuwa "Taarifa rasmi kuhusu uwanja wa mchezo wa marudiano wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika itatolewa baada ya mchezo wa awali utakaochezwa Jumamosi Mei 17, 2025."