Monday , 30th Jun , 2025

Kesi ya mke wa Mpaluka Said Nyagali (Mdude), Sije Emmanuel Mbigi dhidi ya IGP wa Tanzania na wenzake wa 5, Na. 14538/2025, katika Mahakama Kuu kanda ya Mbeya,

Kesi ya mke wa Mpaluka Said Nyagali (Mdude), Sije Emmanuel Mbigi dhidi ya IGP wa Tanzania na wenzake wa 5, Na. 14538/2025, katika Mahakama Kuu kanda ya Mbeya, inaendelea kusikilizwa mahakamani hapo, huku kiini cha kesi hiyo ni kuwa mwombaji pamoja na Mambo mengine anaiomba mahakama Kuu kuwaamuru wajibu maombi wakiongozwa na IGP kumuachia huru mumewe Mdude au kumfikisha mahakamani na kumfungilia mashitaka kwa mujibu wa sheria.

Mdude ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu na utawala wa sheria na mfuasi wa Chadema alivamiwa, kupigwa na kutoweka naye nyumbani kwake mtaa wa Lwambi Jijini mbeya mnamo tarehe 2 Mei, 2025 na watu waliojitambulisha kama askari polisi na mpaka sasa hajapatikana huku jeshi la polisi likikana kumshikilia.