
Waziri alikuwa amesema hakuna kitu kama "ombaomba" nchini Cuba na watu wanaopitia takataka walikuwa, kimsingi, wakifanya hivyo kwa hiari ya kupata "fedha rahisi", kama alivyoelezea.
Maoni yake, yaliyotolewa katika kikao cha bunge, yalikasolewa na Wacuba ndani na nje ya nchi, na kulaumiwa na rais wa kisiwa hicho, Miguel Díaz-Canel.Alilazimika kujiuzulu hivi karibuni
Viwango vya umaskini na uhaba wa chakula vimezidi kuwa vibaya nchini Cuba huku ikiendelea kukabiliwa na mzozo mkubwa wa kiuchumi
Feitó Cabrera alitoa maoni hayo mapema wiki hii katika kikao cha Bunge la Kitaifa.
"Hakuna ombaomba nchini Cuba. Kuna watu wanajifanya ombaomba ili kupata pesa kirahisi," alisema.
Katika kujibu madai yake kwamba hakukuwa na ombaomba nchini Cuba, lakini watu waliojigeuza kuwa ombaomba, mwanauchumi wa Cuba Pedro Monreal aliandika kwenye X: "Lazima kuna watu pia waliojificha kama 'mawaziri'".