Friday , 25th Jul , 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaomba watanzania kuendeleza uzalendo kwa kulinda uhuru, amani na mshikamano waliouacha mashujaa kwa taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaomba watanzania kuendeleza uzalendo kwa kulinda uhuru, amani na mshikamano waliouacha mashujaa kwa taifa.

Katika chapisho aliloliandika kwenye mtandao wa X zamani Twitter Rais Samia amesema kuwa Julai 25 kila mwaka ni siku muhimu kwa Taifa, Siku ya Mashujaa, ambapo Watanzania huungana kuwakumbuka na kuwashukuru wale wote waliotoa maisha yao kupigania uhuru na kulinda amani na heshima ya nchi.

“Tunaendelea kuwaombea wapumzike kwa amani. Tunapowaenzi mashujaa wetu, sote kwa pamoja tuendelee kukumbuka pia wajibu wetu wa kubaki kuwa wazalendo kwa nchi yetu, kulinda uhuru, amani, utulivu na mshikamano waliotuachia wale waliotutangulia, huku tukifanya kazi kwa bidii kwa maendeleo ya Taifa letu”ameongeza.

Maadhimisho hayo kwa mwaka huu yamefanyika katika viwanja vya Mashujaa vilivyopo makao makuu ya nchi, mjini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini na serikali.