Thursday , 7th Aug , 2025

Rais wa Kenya William Ruto amesema taifa hilo halitaacha kushirikiana na China kibiashara licha ya washirika wake kadhaa kuonesha kulalamikia uhusiano wa mataifa hayo

Rais Ruto amekiri kuwa baadhi ya washirika wake wanahoji ukuaji wa kibiashara kati ya Kenya na China lakini akasisitiza kuwa maamuzi ya hatua hizo yanashinikizwa na mahitaji ya Kenya kiuchumi.

"Baadhi ya marafiki zetu wanalalamika kwamba tunafanya biashara nyingi na China. Wakati nilikutana na Rais Xi Jinping, nilimwambia Kenya inaingiza bidhaa za Sh600 bilioni kutoka China, lakini tunasafirisha tu labda 5%. Usawa huo wa kibiashara ni mbaya," Ruto alisema.

Ruto aliongeza kuwa China imekubali kufungua soko lake kwa bidhaa za kilimo za Kenya.

“Wamekubali kufanya ya mabadiliko ya usawa wa kibiashara katika ya Kenya na China. Wamekubali kuondoa ushuru wote kwa chai yetu, kahawa, parachichi na bidhaa zote za kilimo tunazouza nje ya nchi. #EastAfricaTV