Monday , 8th Sep , 2025

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imesema katika kipindi cha Mwezi Julai na Septemba 7/ 2025 Mamlaka hiyo imefanikiwa kukamata kilogramu 33,077.613 za dawa za kulevya aina mbalimbali, kilogramu 4,553 za mbegu za bangi pamoja na kuteketeza mashamba ya bangi ekari 64

Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imesema katika kipindi cha Mwezi Julai na Septemba 7/ 2025 Mamlaka hiyo imefanikiwa kukamata kilogramu 33,077.613 za dawa za kulevya aina mbalimbali, kilogramu 4,553 za mbegu za bangi pamoja na kuteketeza mashamba ya bangi ekari 64. 

Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Septemba 8, Kamishina Jenerali Aretas Lyimo amesema Sambamba na hayo DCEA wamekamata silaha mbili za moto aina ya gobore na bastola ikiwa na risasi 11, magari tisa (9), bajaji 2 na pikipiki 26 zilizohusishwa kwenye uhalifu huo huku watu 940 wakikamatwa baada ya husishwa na matukio hayo.

Katika operesheni iliyofanyika jijini Dar es Salaam, mtaa wa Tupendane - Manzese Wilayani Ubungo walikamata watu watatu akiwemo raia wa Lebanon, wakiwa na kilogramu 2.443 za dawa za kulevya aina ya cocaine.

Dawa hizi ziliingizwa nchini kutokea nchini Brazili kupitia nchini kenya, na baadaye kwenda Uganda na kisha kuingizwa Tanzania kupitia njia za vipenyo.