Tuesday , 16th Sep , 2025

Rais wa Marekani Donald Trump amewasili Uingereza kwa ziara rasmi ya siku mbili ambapo serikali ya Uingereza inatumai kusaini mkataba wa kiteknolojia wenye thamani ya mabilioni ya dola.

Ziara ya Trump inafanyika wakati vita vinaendelea Ukraine na Mashariki ya Kati, mataifa makubwa yakikabiliana na ushuru wa Marekani, na hii leo Uingereza ina matumaini kuwa maonesho ya kifalme yaweza kumvutia Trump na kumuweka upande wao.

Trump amekuwa akivutiwa na familia ya kifalme kwa muda mrefu na ameandaliwa mapokezi ya msafara wa gari la kifahari akiwa na Mfalme Charles III pamoja na karamu kubwa ya kitaifa katika Kasri la Windsor.

Kiongozi wa chama cha Labour, Kier Starmer, si mshirika wa kawaida wa kisiasa wa Trump mwenye mrengo mkali wa kulia, lakini amekuwa akijitahidi kumvutia tangu alipochaguliwa tena kuwa Rais mwezi Januari.

Starmer alimpa mwaliko rasmi kutoka kwa mfalme katika Ikulu ya White House mwezi Februari. Trump alikubali mwaliko na kumwambia Starmer kuwa Mfalme Charles, ambaye kwa sasa anapata matibabu ya saratani ni mtu mzuri sana.

Olivia O'sullivan mchambuzi wa siasa za Uingereza anasema "Sawa, ulikuwa mwaliko muhimu kwa Uingereza, si kawaida kutoa mwaliko wa ziara ya pili ya kitaifa kwa mkuu wa taifa. Lakini Uingereza inatamani kuhakikisha kuwa inaweza kupata jambo la kimkakati na lenye maana kutoka kwenye ziara hii.