Monday , 17th Nov , 2025

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya iliyotolewa jana November 16 imeeleza kuwa Ongeta alikamatwa wakati akijaribu kuingia Tanzania kwa kutumia gari lenye namba za usajili KDP 502 Y aina ya Toyota Landcruiser.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya limemkamata Charles Onkuri Ongeta (30) mwenye uraia pacha wa Marekani na Kenya ambaye ni mwanajeshi wa Marekani mwenye cheo cha Sajenti akiwa na mabomu ya aina ya CS M68 ya kurushwa kwa mkono katika mpaka wa Tanzania na Kenya-Sirari.

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya iliyotolewa jana November 16 imeeleza kuwa Ongeta alikamatwa wakati akijaribu kuingia Tanzania kwa kutumia gari lenye namba za usajili KDP 502 Y aina ya Toyota Landcruiser.

“Mabomu hayo kwa mujibu wa sheria ya umiliki wa silaha hata kama angeomba kibali cha kuingia nayo nchini asingeruhusiwa”imepainisha taarifa hiyo.

Kufuatia tukio hilo, jeshi la polisi limesema linaendelea kukusanya Ushahidi na kumhoji bwa na Ongeta kabla ya hatua za kisheria kuchukuliwa juu yake.