Monday , 24th Nov , 2025

Mchambuzi wa soka na beki wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher, amemuomba radhi nyota wa Arsenal Eberechi Eze, kufuatia kauli yake kabla ya mechi ya ‘Dabi ya Kaskazini mwa London’.

Jamie Carragher na Eberichi Eze

Eberechi Eze aliiwezesha Arsenal kupata ushindi wa mabao 4-1 Tottenham Hotspur katika ‘Dabi ya Kaskazini mwa London’ jana Jumapili, Novemba 23, akifunga mabao matatu, huku Trossard akifunga bao la kwanza.

Carragher alitoa kauli hiyo katika kipindi chake cha uchambuzi akidai kuwa, mchezaji huyo asingekuwa na mchango mkubwa wa kuamua matokeo ya mechi kubwa. Hata hivyo, baada ya Arsenal kuibuka na ushindi mkubwa, gwiji huyo amekiri kuwa kauli yake haikuwa sahihi na ameomba radhi.

"Ningependa kuomba radhi kwa Eberechi Eze. Baada ya kuona jinsi alivyocheza na kuisaidia Arsenal kupata ushindi mnono, ninakiri nilikosea kutamka maneno yale. Eze amenithibitishia kwa vitendo dhidi ya Tottenham," amesema Carragher

Ushindi huo wa 4-1 unaipa Arsenal kuendelea kubaki kileleni mwa Ligi Kuu ya EPL, huku mashabiki wakipomngeza nyota huyo aliyesajiliwa klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu akitokea Crystal Palace kwa ada ya Pauni 67.5 milioni