Tuesday , 2nd Dec , 2025

Novemba 30 majira ya saa moja usiku kwa kuchomwa na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mapajani, shingoni na kichwani.

Askari wa Jeshi la Magereza mwenye umri wa miaka 31 (jina limehifadhiwa) anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga akituhumiwa kumuua mpenzi wake, Bitie Chacha (25), mwalimu wa Shule ya Msingi, mkazi wa Bugweto A, Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi Bitie aliuawa Novemba 30 majira ya saa moja usiku kwa kuchomwa na kisu sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo mapajani, shingoni na kichwani.

Kabla ya kuhitilafiana Bitie alikuwa akiishi na ofisa magereza huyo kama wapenzi lakini ilitokea kutokuelewana kati yao ndipo mtuhumiwa akamshambulia mwalimu huyo.

Kwa mujibu wa rafiki yake na marehemu, ugomvi wa wapenzi hao ulianzia baa baada ya askari huyo kuchukua simu ya mkononi ya marehemu na kusoma ujumbe mfupi.