Watu watano wamefariki dunia katika ajali ya Helkopta ya kampuni ya uokoaji ya KiliMediaur Aviation kwenye hifadhi ya mlima Kilimanjaro maeneo ya kati ya Kibo na Barafu Camp.
Helkopta hiyo ilipata ajali wakati inatoka kuchukua wagonjwa katika hifadhi mlima Kilimanjaro waliopanda kupitia kampuni ya Utalii BobyCamping.
Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro,SACP Simon Maigwa amesema kuwa ajali hiyo imetoka jana Desemba 24, saa 11:30 ikiwa inatoka kuchukua wagonjwa wa kampuni ya Utalii BobyCamping.
Maigwa amewataja waliofariki katika ajali hiyo ya Helkopta ya kampuni ya uokoaji KiliMediaur kuwa ni Wageni wawili, Tour Guide (Muongoza watalii) mmoja,Rubani mmoja na Daktari mmoja.
Eneo la Kibo Hut na Barafu Camp ni urefu wa kati ya meta 4,670 na meta 4,700 kutoka usawa wa bahari.
