Sunday , 28th Dec , 2025

Mtuhumiwa huyo amekamatwa katika eneo la Kihonda Kwachambo, barabara kuu ya Morogoro–Dodoma, ambapo polisi walilazimika kumzuia kuendelea na safari kwa ajili ya usalama huku kipimo kikionyesha ulevi wa 171.7mg/100ml.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limemweka chini ya uangalizi dereva Uwimpue Bonheur (33), raia wa Kigali, Rwanda, baada ya kukamatwa akiendesha lori la mizigo aina ya HOWO lenye namba RAI 878 G akiwa amelewa kupita kiasi.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa katika eneo la Kihonda Kwachambo, barabara kuu ya Morogoro–Dodoma, ambapo polisi walilazimika kumzuia kuendelea na safari kwa ajili ya usalama huku kipimo kikionyesha ulevi wa 171.7mg/100ml.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama ametoa ushauri kwa madereva kuepuka kuendesha katika hali ya ulevi ili kuokoa maisha ya watu na kuepusha ajali huku akibainisha kuwa hatua za kisheria dhidi ya dereva Uwimpue Bonheur zinaendelea.