Wednesday , 31st Dec , 2025

Ushirikiano huo umefanyika leo Jumatano Disemba 31 kwenye jengo la Utawala lililopo katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mtajirishaji Media Group Interprises(MMGE) kwa kushiriakiana na Chuo kikuu cha Dar es Salaam, wamesaini mkataba wa ushirikiano wa kutoa ujuzi na kukuza soko la ajira katika sekta mbalimbali kwa vijana na Mama lishe maarufu kama ‘’Mama Ntilie’’ lengo kubwa ni kuwawezesha kibiashara na kutoa elimu.

Ushirikiano huo umefanyika leo Jumatano Disemba 31 kwenye jengo la Utawala lililopo katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Mara baada ya kusaini mkataba wa Mwanzilishi Mwenza wa Edmund Libent Kaiza, amesema ushirikiano huo utakuwa na matokeo chanya kwa vijana na Mama Lishe ambao ndio walengwa wakuu, huku wakihakikisha wenye utaalam au ujuzi wanafungamanishwa na wenye fursa ili kuanzisha kampuni na kuondoa kabisha tatizio la ajira nchini.

Aidha, Edmund amesema kupitia ubia huo, Mama lishe watapata elimu ya kuweza kuendesha biashara yao na kuwezeshwa kimtaji kutokana na kupitia changamoto hiyo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa chuo Kikuu ch Dar es Salaam Profesa William Anangisye amesema kupitia ubia huo Wanafunzi wa chuo hicho watanufaika ikiwemo kupata elimu ya kujiajiri ili kupambana na tatizo la ajira nchini.