Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Januari 6 mwaka huu, amekutana na kufanya mazungumzo viongozi mbalimbali wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Katika taarifa iliyotolewa leo na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa viongozi aliokutana nao ni pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda pamoja na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele.
Mazungumzo hayo ambayo pia yamehudhuriwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka yamefanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar.



