Wednesday , 7th Jan , 2026

Chelsea imetangaza Liam Rosenior kuwa kocha mkuu wa timu hiyo, akisaini mkataba wa kudumu hadi mwaka 2032.

Liam Rosenior

Rosenior, ambaye alikuwa kinara katika mchakato wa kuwania nafasi ya ukocha klabuni hapo baada ya kuondoka kwa Enzo Maresca, amekabidhiwa jukumu la kuiongoza Chelsea ambayo ianhamu ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya England, na michuano mingine mikubwa ya ndani na kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chelsea, kocha huyo amesaini mkataba wa muda mrefu ili kukidhi haja ya klabu hiyo ya jijini London, ambayo imejipanga kuwa na kikosi imara na chenye ushindani ambacho kitakua na mipango ya kutwaa mataji kwa siku za usoni.

Rosenior amejiunga na Chelsea akitokea RC Strasbourg inayoshiriki Ligi ya Ufaransa Ligue 1. Kocha huyo ameiacha RC Strasbourg ikiwa nafasi ya saba katika ligi ya Ufaransa.