Tuesday , 13th Jan , 2026

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 5195 ya mwaka 2025 katika Hakimu Mkazi Kisutu.

Wafanyabiashara sita wanaokabiliwa na kesi ya kuwasilisha nyaraka za uongo katika Bandari ya Dar es Salaam na kujipatia zaidi ya Sh10 bilioni zilizotokana na shehena ya mafuta watasomewa maelezo ya mashahidi na vielelezo na Jamhuri imepanga leo Jumanne, Januari 13, 2026 baada ya upelelezi wa kesi hiyo ya uhujumu uchumi kukamilika.

Wanaoshtakiwa katika kesi hiyo ni Joseph Matage; Grace Matage ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya RHG General Traders Ltd na pia ni wakala wa forodha; Jamaal Saad; Mubinkhan Dalwai; Stanley Tibihenda na Edward Omeno ambao wote ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi namba 5195 ya mwaka 2025 katika Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo ina jumla ya mashtaka 13 yakiwamo ya kula njama, kuwasilisha nyaraka za uongo katika Bandari ya Dar es Salaam na kujipatia Sh10 bilioni zilizotokana na shehena ya mafuta.