Monday , 19th Jan , 2026

Unaambiwa rapa The Game alikuwa tayari kupoteza maisha yake wakati wapo kwenye bifu zito na 50 Cent!

Picha ya msanii 50 Cent na The Game

Kwenye interview aliyofanya na Vibe Magazine, The Game anasema 

"Nilikuwa tayari nimejiandaa kufa kipindi tuna bifu na 50 Cent. Nina uhakika kwa asilimia mia mimi na 50 Cent tulikuwa tunaenda kufa kwa sababu tumeona vitu hivyo vimetokea".

"Alikuwa rapa mkubwa kutoka East, mimi mkubwa kutoka West na tulikuwa bado vijana nilisema liwalo na liwe. Nilikuwa namchukia sana alipojaribu kunichezea, kama Biggie na Pac wamekufa nikasema inaweza kutokea kweli".

Bifu la lao lilianza mwaka 2005 baada ya The Game kuachia Album yake ya kwanza 'The Documentary' 50 Cent akaibuka kusema hakuthaminiwa wala kupewa Credit sababu aliandika nyimbo nyingi kwenye Album hiyo.