Thursday , 2nd Jul , 2026

Muimbaji wa South Africa na mshindi wa tuzo za Grammy mara 2 Tyla amesainiwa na kampuni ya burudani ya Roc Nation inayomilikiwa na rapa Jay Z.

Picha ya Tyla na Jay Z

Tyla ameingia mkataba huo wa usimamizi wa kazi zake za muziki, brand, uhusiano wa ndani na nje ya career yake ambao utakuwa na faida kubwa katika safari yake ya muziki duniani.

Ushirikiano huo kati ya Tyla na Roc Nation ulitangazwa kupitia mabango makubwa yaliyotawala eneo la Times Square jijini New York na ujumbe unaosomeka 

"Roc Nation tunamkaribisha Tyla kwenye familia"

Baadhi ya wasanii ambao wapo na waliopita Roc Nation ya Jay Z ni Rihanna, Alicia Keys, DJ Khaled, J Cole, Megan Thee Stallion, ASAP Rocky, John Legend, Big Sean, Fat Joe, Jadakiss, Ayra Starr na J Balvin.