Saturday , 11th Jul , 2026

 Nyota wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Mamelodi Sundowns, Jayden Adams amefariki Dunia akiwa na umri wa miaka 25, ikiwa ni muda mfupi tu baada ya kuiwakilisha Bafana Bafana kwenye michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Jayden Adams

Adams, pamoja na wachezaji wengine saba wa Mamelodi Sundowns walioiwakilisha Afrika Kusini kwenye Kombe la Dunia, walipewa likizo ya wiki mbili zaidi kabla ya kurejea kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya na alitarajiwa kujiunga tena na kikosi cha klabu hiyo wiki ijayo kwa ajili ya kambi ya mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya huko Austria.

Kiungo huyo ambaye ni zao la akademi ya Stellenbosch alikuwa sehemu ya kikosi cha Bafana Bafana kilichoshinda medali ya shaba kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2024) huko Ivory Coast

Chanzo rasmi cha kifo cha Jayden Adams bado hakijathibitishwa rasmi na mamlaka za kiserikali, familia yake, au klabu ya Mamelodi Sundowns