
Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ambapo atasaidiwa na Anold Bugado (Singida), Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam)
Huku Kamishna wa mechi hiyo Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza ambao wote ni waamuzi wamesoma na wanajua sheria 17 za soka na hivyo amewataka mashabiki kuwa watulivu na kushangilia timu zao kwa amani badala ya kuingilia maamuzi ya waamuzi hao.
Na kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya Azam FC afisa habari wa Yanga Baaraka Kizuguto amesema kuwa mchezo huo ni kama fainali kwao na kwakulitambua hilo wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi hapo kesho na kupunguza wigo wa pointi baina ya timu hizo mbili.
