Waziri Mkenda aweka wazi mchakato wa Mitaala mipya
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda amesema Serikali ina mpango kabambe wa kukimbiza na kuyafanyia haraka mageuzi ya elimu ambapo kufikia mwezi Disemba 2022 rasimu ya Mitaala mipya pamoja na rasimu ya mapitio ya sera itakuwa imekamilika.