Mbunge ataka Kisukuma kiwe lugha ya biashara
Mbunge wa jimbo la Mbogwe Nicodemas Maganga, amesema Tanzania inabidi ichague lugha kutoka kwenye kabila moja hapa nchini ikiwemo Kisukuma kwa ajili ya kuiweka kwenye system itakayopelekea Wachina ama Wazungu watakapokuja nchini waisomee na itumike katika biashara.