Watumishi 14 wa AMCOS wafukuzwa kazi
Watumishi 14 ambao ni Wahasibu wa Vyama vya msingi vya Ushirika (AMCOS) Wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, wamefukuzwa kazi huku afisa mwingine mmoja akichunguzwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kufuatia tuhuma mbalimbali ikiwemo ubadhilifu wa fedha.