Wawili Real Madrid kuikosa PSG
Mabingwa wa kihistoria wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, Real Madrid itawakosa nyota wake kiungo Casemiro na beki wa kushoto Ferland Mendy kwenye mchezo wa 16 bora wa michuano hiyo dhidi ya PSG ya Ufaransa utakaochezwa saa 5:00 usiku wa leo.

