Ajinyonga baada ya kumchinja mke wake
Mwanaume mmoja mkazi wa kijiji cha Mtakuja, Kata ya Nsekwa wilaya ya Mlele mkoani Katavi anayejulikana kwa jina la Anisent John mwenye umri wa miaka 32 amemchinja mkewe kwa panga sehemu ya shingoni kisha na yeye kujinyonga kwa kutumia chandarua.

