Mkuu wa Shule atafuna ada, Serikali yamjia juu
Serikali mkoani Geita imeuagiza uongozi wa shule ya sekondari ya Geita Islamic, ifikapo kesho asubuhi iwasilishe stakabadhi za malipo ya mitihani ya wanafunzi, baada ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo kukiri kula ada za mitihani ya Taifa ya wanafunzi wa kidato cha Pili na cha Nne.